Kiwanda kikubwa na cha kwanza kutengeneza na kuunganisha Magari nchini Tanzania GF vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimetimiza utengenezaji wa gari ya miamoja (4000) tangu kuanza uzalishaji rasmi wa kiwanda hicho 2020.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuruhusu gari ya 4000 kukanyaga ardhini baada ya kuunganishwa tayari kwa kutembea, Meneja mkuu wa kiwanda hicho, Ezra Mereng alisema wanaishukuru serikali kupendekeza Tozo ya maendeleo ya viwanda kwenye vichwa vya Terla za magari makubwa vinavyoagizwa nchini kwa asilimia 10 ili kuvilinda viwanda vya ndani na kuchochea ununuzi wa magari yalionunganishwa nchini alimaliza manger

Kwa upande wa Mkurugenzi wa GFA, All Jawad Karmali amesema wao wamejipanga katika kuhakikisha wanaongeza mtaji katika uwekezaji ili kukabiliana na soko la Afrika mashariki na kati kwa upande wa magari na Tanzania kuwa nchi mojawapo inayounganisha magari na kulisha ukanda wote wa Afika mashariki na hii inatokana na mazingira mazuri ya serikali kwa wawekezaji nchini
Pia alizitaka tasisisi za serikali na kuagiza magari ambayo hayajaunganishwa na kazi ya kuunganisha ifanyike na viwanda vya ndani ili kukuza pato la taifa na kuongeza ajira kwa watanzania, pia kama nchi itajipatia fedha za kikgeni kwa kuuza nchi jirani magari yanayotoka Tanzania.