Latest Posts

KUUTAKA UBUNGE KUMEWAPONZA?

Jumanne Machi 11, 2025 akiwa jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwataka Wakuu wa Wilaya(DC), Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) na watumishi wengine wa umma wanaotaka kugombea katika nyadhifa mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu watoe taarifa mapema ili nafasi zao ziweze kupata watu watakaozishikilia.

Katika mkutano huo Rais Samia aliawaeleza kuwa endapo hawatatoa taarifa basi huenda wakakosa nafasi za kuchaguliwa na wakikosa hawatapata nafasi ya kurudi katika utumishi wa umma.

Hata hivyo alieleza sababu kubwa ya kutoa agizo hilo mapema ni ili wapatikane watakaoshika nafasi zilizoachwa wazi mapema.

Jana juni 23, 2025 taarifa ya uteuzi wa Wakuu wa mikoa na wilaya imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu naomba nikupitishe katika teuzi kadhaa zilizotikisa.

Kenan Kihongosi amehamishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambao ulikuwa chini ya Paul Makonda.

Paul Christian Makonda 2020 alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam baadae akaenda kutia nia ubunge jimbo la Kigamboni ambapo alishindwa kwenye kura za maoni. Mwaka huu Makonda alikua Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo siku za karibuni pamekuwa na kuvutana na kupigana vijembe vya kisiasa baina yake na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo jamno ambalo ilidhaniwa ni ‘analitaka jimbo’.

Ikumbukwe siku za karibuni akizungumza mbele ya Waziri Mkuu yeye(Makonda) alimtakia heri Waziri Mkuu akisema anamuombea huku akimuomba PM naye amuombee ikiwezekana wakutane mahala fulani(bungeni).

Uteuzi wa Kheri James Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Mkoa huu ulikuwa unaongozwa na Peter Serukamba ambaye yeye hakutana kuficha siku miezi takribani miwili nyumba alisema kuwa anautaka ubunge na hataki kuficha hilo. Uteuzi wa Kheri huenda umekwenda kukamilisha mchakato huo.

Uteuzi wa Jabiri Makame kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Mkoa huu ulikuwa unaongozwa na Daniel Chongolo ambaye amekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (2021-2023) naye hakuna taarifa ya kahamishiwa wapi japo hakuwahi kuonyesha hadharani nia yake ya ubunge.

Masanja Kadogosa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TRC naye nafasi yake imechukuliwa na Mhandisi Machibya Masanja. Kadogosa amekuwa akitajwa kwa muda sasa kuwa analitaka jimbo la Bariadi vijijini.

Hawa ni baadhi ya wale walioonyesha nia kuondolewa katika nafasi zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!