Latest Posts

MABONANZA YA MARA KWA MARA YATASAIDIA KUZUIA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZI

 

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesisitiza umuhimu wa kuandaa mabonanza ya mara kwa mara kwa watumishi wa wizara ili kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoyakuambukiza.

 

Akizungumza katika Madini Bonanza lililowajumuisha Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zaken lililofanyika leo Jumamosi Oktoba 19,2024 Jijini Dodoma, Waziri Mavunde ameeleza kuwa magonjwa haya, yakiwemo kisukari na shinikizo la damu, yamekuwa changamoto kubwa nchini, hasa kwa watumishi ambao hawajishughulishi na mazoezi.

 

Amesema, “Asilimia kubwa ya watumishi wamekuwa na uzito na wanafanya mazoezi kidogo. Wakati mwingine, tunatoka kwenye magari yetu na kuelekea kwenye viti ili kuangalia televisheni, hali inayoweza kupelekea magonjwa.”

Aliongeza kuwa, kufanya mazoezi ni muhimu kwa afya na kwa ufanisi wa kazi katika wizara.

Amesema bonanza hilo lililenga kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi wa wizara na taasisi zake huku akisisitiza kuwa ushirikiano ni muhimu katika kuendesha sekta ya madini, na kuonyesha kwamba wizara imepata maendeleo mazuri na changamoto nyingi zinaendelea kutatuliwa.

 

“Ni muhimu kuendeleza tabia ya kufanya mazoezi ili kuboresha afya na ufanisi wa kazi miongoni mwa watumishi wa wizara, amesema

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Terence Ngole, ameeleza kuhusu mashindano mbalimbali ya michezo yaliyofanyika, ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu na mbio za mita 100 na 400.

 

Ngole amefafanua kuwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) iliondoka na medali nyingi na makombe kutokana na ushindi huo.

 

Ngole pia ameongeza kuwa asilimia 5 ya Watanzania wanakabiliwa na magonjwa yasiyoambukiza, na hivyo mabondanza kama haya ni muhimu kuhamasisha watumishi kufanya mazoezi na kuboresha afya zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!