Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linawashikilia watu 192 kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya, uvuvi haramu na utengenezaji wa pombe haramu aina ya gongo, kutokana na oparesheni maalum zilizofanyika kwa nyakati tofauti katika mkoa huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Pius Lutumo, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na mali haramu zikiwemo bangi kilo 1,103, mirungi kilo 65, nyavu haramu 515 na pombe ya moshi (gongo) lita 1,320
ACP Lutumo amesema mashauri ya watuhumiwa hao yako katika hatua mbalimbali za upelelezi ndani ya mnyororo wa haki jinai.
Kamanda Lutumo pia amewataka wananchi kuzingatia Tangazo la Serikali Na. 537 la Agosti 29, 2025, linalotaka wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha katika vituo vya polisi au ofisi za watendaji wa serikali kabla ya Oktoba 31, 2025.