Mashindano ya mpira wa kikapu kwa wanaume katika michezo ya majeshi nchini yanaendelea kwa kiwango cha juu cha ushindani, huku timu tatu za SMZ, Magereza na JKT zikionesha umahiri mkubwa.
Mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), mkoani Morogoro, yamewakutanisha timu sita, ikiwemo Uhamiaji, Polisi, Ngome, SMZ, Magereza, na JKT.
Katika mechi za hivi karibuni, timu tatu zimeibuka washindi: Polisi walishinda kwa pointi 63 dhidi ya Uhamiaji waliopata 52, Magereza walishinda kwa pointi 78 dhidi ya SMZ waliopata 44, na JKT walishinda kwa pointi 58 dhidi ya Ngome waliopata 57, na hivyo kuondoka na alama tatu muhimu.
Mwalimu wa mpira wa kikapu kanda wa Magereza, Joseph Matley amesema kwamba malengo makubwa ya timu yao ni kuhakikisha wachezaji wanacheza kwa kufuata maelekezo na kujituma uwanjani hii imesababisha mchezo kuwa wa kuvutia na wa kufurahisha kwa watazamaji.