Latest Posts

MASWALI MATANO YA ACT WAZALENDO KWA RAIS SAMIA

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa msimamo wa hivi karibuni wa serikali ya awamu ya sita (6) chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuamua kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa usimamiwe na TAMISEMI (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) badala ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na kutoa nafasi kwa wajumbe wa sasa wa tume hiyo kuendelea na majukumu yao unazalisha maswali matano (5) ambayo serikali ni lazima inapaswa kutambua kuwa ina wajibu wa kuyajibu

Ado ametoa kauli hiyo akiwa kwenye mkutano mkuu wa ACT Wazalendo wa kata ya Azimio, iliyopo jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, mkutano uliofanyika Juni 24.2024 ambapo miongoni mwa maswali hayo ni pamoja na;

i) Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iko wapi; katika kujenga hoja ya swali hilo Ado amehoji inakuwaje na Tume Huru ya ya Taifa Uchaguzi (INEC) bila mabadiliko ya wajumbe wa tume wataopatikana kwa utaratibu mpya wa usaili, ambapo ameuliza endapo ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuleta mageuzi ya kisiasa nchini ilikuwa ni kubadili tu jina la Tume ya Uchaguzi au kubadili pia muundo na watendaji wa tume hiyo

Amesisitiza kuwa hatua muhimu ya kuanzia katika kupata Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilikuwa ni kwa wajumbe wa sasa wa tume hiyo kujiuzulu ili kupisha uteuzi wa wajumbe wapya, amedai kuwa wajumbe wengi wa sasa wa tume hiyo hawana uhalali wa kimaadili kusimamia uchaguzi kwa sababu wameshiriki kuharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na chaguzi za marudio zilizofanyika katika miaka minne iliyopita

ii) Swali la pili alilohoji Ado Shaibu ni kwamba uchaguzi huo unaotarajiwa kusimamiwa na TAMISEMI (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) badala ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ni wa serikali za mitaa au ni uchaguzi wa CCM (Chama cha Mapinduzi)?

Amehoji, ikiwa uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba 2024 ni uchaguzi wa serikali za mitaa kwa nini serikali inang’ang’ania usimamiwe na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Ofisi ya Rais -TAMISEMI) ambayo inaongozwa na Waziri Mohamed Mchengerwa ambaye anafahamika wazi kuwa ni kada wa chama tawala (CCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho?

iii) Ado Shaibu ameelekeza swali la tatu kwa Rais Samia akihoji kwa nini serikali haitaki kutekeleza sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi?

Amesema kulikuwa na ulazima gani wa kutunga sheria ya kuipa mamlaka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa halafu baadaye sheria hiyo kupuuza utekelezaji wake, amesema kwa nini serikali haitaki kupeleka muswada Bungeni wa kutekeleza kifungu cha 10(1)(c) ili uchaguzi ujao wa serikali za mitaa usimamiwe na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)?

iv) Aidha, Ado Shaibu amehoji endapo ipo nia ya dhati ya kusafisha daftari la kudumu la wapiga kura nchini

Amesema chama cha CT Wazalendo kimefanya uchambuzi wa awali wa daftari la kudumu la wapiga kura, na kujiridhisha kuwa daftari hilo limechafuliwa sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ambapo amedai kuwa watu wengi wasio na sifa wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura lakini ameenda mbali zaidi na kueleza kuwa INEC haina nia ya kulisafisha daftari ipasavyo, hivyo kumuhoji Rais Samia ni lini daftari hilo litasafishwa, na je ni nani watakaofanya kazi hiyo

v) Swali la tano na la mwisho alilohoji Ado Shaibu (,Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo) kwa Rais Samia ni kuhusiana na falsafa ya 4Rs, ambayo imeasisiwa na yeye mwenyewe (Rais Samia) kama imekufa au la?, na kama jibu la swali hilo ni ndio je, ndo tunarudi tulikotoka (miaka ya nyuma)?

Amesema kwa mwenendo wa sasa wa serikali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, falsafa ya 4R’s iliyokusudia kufungua ukurasa mpya wa kisiasa imekufa na sasa amedai kuwa ni rasmi nchi inarejea kwenye mazingira yaliyokuwepo kwenye uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!