

Theophilida Felician Kagera.
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini mkoani Kagera Mhe Eng Johnston Mutasingwa ameelezea namna anavyoguswa na mchango mkubwa wa waandishi wa habari unavyochangia pakubwa ujenzi wa maendeleo nyanja mbalimbali kupitia kalamu zao.
Mhe Mutasingwa ametoa kauli hiyo akishiriki chakula cha mchana na waandishi wa habari Manispaa ya Bukoba ambapo awali amepongeza nguvu kazi ya waandishi wa habari na vyombo vya habari vilivyoko ndani na nje ya Bukoba kwa namna vinavyojimudu na kutangaza habari maeneo mbalimbali hatimaye kuitangaza Bukoba na Kagera.
Amefafanua kwamba sekta ya habari ni kiungo muhimu katika ujenzi wa maendeleo ya jamii pale inapotumika vyema kwakufuata misingi na maadili ya taaluma hiyo hivyo ni matajirio yake kuwa waandishi wa habari wataendelea kuwa nyenzo imara katika uchapakazi wao wakuijenga Bukoba.
Hata hivyo amesisitiza neno la kuwapa ushirikiano waandishi wa habari ili kuhakikisha safari ya ujenzi wa maendeleo inakwenda kasi huku akiwasihi kutumia kalamu zao vizuri kwakuhamasisha mambo muhimu ikiwemo kuitunza amani nakuzichangamkia fursa mbalimbali zenye kuwainua kiuchumi.
Naye mstahiki meya wa Manispaa ya Bukoba Mhe Action Lwankomezi akiambatana na mbunge huyo ameshukuru nguvu ya waandishi wa habari naye akiahidi kuwa nao bega kwa bega kwakutumia vyombo vyote vya habari vya ndani na nje ya Bukoba.
Aidha waandishi wa habari kwa pamoja wamemshukuru na kumpongeza mbunge Mtasingwa kuona umuhimu wa kutenga muda wake na kukutana na kundi hilo jambo ambalo hawakusita kusema wazi mbele yake kuwa limewafariji kwani haikizoeleka kwao vipindi vingine vilivyopita wabunge kutenga muda na kukutana nao katika kuyateta mambo muhimu kama ilivyojiri kwa Mhe Mutasingwa hivyo wamemuahidi ushirikiano zaidi.