Mkuu wa Morogoro Adam Malima amesema mashindano ya michezo ya baraza la michezo ya majeshi yatakayotimua vumbi mkoani Morogoro kuanzia Septemba 6 hadi 15 yatasaidia kuleta umoja miongoni mwa vikosi vya majeshi nchini na kuibua vipaji vilivyomo ndani vikosi hivyo.
Malima ameyasema hayo mkoani humo katika kikao cha wajumbe wa baraza la michezo ya majeshi Tanzania BAMMATA ambapo amesisitiza kuwa ni wakati sasa wa kuibua vipaji katika michezo.
Kwa upande mwenyekiti wa baraza hilo Brigedia Jenerali Said Hamis Said amesema kuwa wameuchagua mkoa wa Morogoro ili kuunga mkono juhudi za Mkoa huo katika kuibua vipaji vya michezo nchini.