Latest Posts

MWANAMKE AHOJIWA NIGERIA KWA KUCHANA PASIPOTI YA MUMEWE UWANJA WA NDEGE

Idara ya Uhamiaji nchini Nigeria inamhoji mwanamke aliyerekodiwa akichana pasipoti ya mume wake katika uwanja wa ndege wa Lagos katika video ambayo imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Favour Igiebor, alionekana akimfokea mume wake kwenye video hiyo huku vipande vya pasipoti ya Nigeria vikiwa chini.

Kwa mujibu wa BBC Swahili, wanandoa hao na watoto walitua katika uwanja wa ndege wa Murtala Mohammed ambapo kisa hicho kilitokea mbele ya makumi ya wasafiri wengine, huku mamlaka ikisema katika taarifa kwamba inachunguza kisa tukio hilo.

“Huduma ya Uhamiaji ya Nigeria (NIS) imeanzisha uchunguzi rasmi, video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha msafiri wa kike akiharibu pasi ya usafiri ya Nigeria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Mohammed (MMIA), Lagos, mtu aliyehusika ametambuliwa kama Bi. Favour Igiebor,” taarifa hiyo ilisema.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa kuharibu pasipoti ya nchi ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni kifungo cha hadi mwaka mmoja gerezani.

Baada ya video hiyo kuibua gumzo mitandaoni, Igiebor aliachia video yake mwenyewe, hakuelezea kwa undani lakini alisema alikuwa akiteseka.

“Angalia macho yangu, mimi hulia sana, watu wananisimanga kwenye mitandao ya kijamii na hawajui ninachopitia, lazima uhoji chanzo cha ugomvi, usiangalie tu kitendo kilichotokea, nina sababu zangu. nimepitia changamoto nyingi za kifamilia”, ameeleza mwanamama huyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!