Latest Posts

NABII MALISA ATABIRI DAWA YA VVU NA SARATANI KUPATIKANA 2025

Mtumishi wa Mungu wa Kanisa la Madhabahu ya Hatma iliyopo Ubungo Nabii Clear Malisa amesema ametoa baadhi ya nadhiri 25 hasa kwa mwaka ujao 2025 ikiwemo dawa ya kutibu magonjwa sugu kama vile Virusi Vya UKIMWI, Saratani na Kisonono.

Ametoa kauli hiyo Disemba 31, 2024 Jijini Dar es salaam ikiwa ni saa chache zimesalia kuufunga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025.

“Nimetoa baadhi ya nabii kama 25 wiki iliyopita kwaajili ya 2025 lakini zipo nabii zingine nyingi za kusisimua na mambo mengine makubwa ambayo yanaenda kutokea” Nabii Malisa

Katika hatua nyingine Nabii Malisa amewaasa Watanzania kwa ujumla kuufunga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka mpya 2024 kwa kumtanguliza Mungu katika nyumba zao za ibada.

Nabii huyo amesema lengo la kuupokea mwaka na Mungu ni kuhakikisha mipango ya kila mmoja Mungu anaibariki kwa mwaka ujao 2025.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!