Latest Posts

NGO’S MTWARA ZALIA KUPUNGUA KWA UFADHILI WA KUTEKELEZA MIRADI YA KIJAMII

Kupungua kwa wafadhili kutoka nje ya nchi kwenye baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’S) kumepelekea kupungua kwa utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kijamii iliyokuwa inatekelezwa na mashirika hayo.

Hayo yamebainishwa Juni 13,2025 na baadhi ya viongozi wa Ngo’s wa wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara kwenye kikao cha kutathimini mchango wa mashirika hayo kwa kipindi cha miaka mitano iliyowakutanisha mashirika  zaidi ya 40 kutoka Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (MTWANGONET) Fidel Luanda amesema changamoto kubwa inayowakabili ni kupungua kwa wafadhili,baadhi ya nchi au wafadhili kubadili taratibu za fadhili na kubadili vipaumbele vyao hali inayopelekea baadhi ya mashirika kushindwa kutekeleza miradi.

“Zamani tulikuwa na miradi ukiangalia hapa tunamashirika takribani 40 miaka ya nyuma unaweza kuta mashirika 35 yana miradi lakini ukiangalia ripoti ya mwaka huu inaonyesha mashirika ambayo yanatekeleza miradi hayazidi 20 hiyo ni changamoto na inaonyesha moja kwa moja kwamba hii imetuathiri yaani nusu ya mashirika ambayo yapo hapa ndo yana miradi lakini mingine hayana fedha na yanategemea fedha za mapato yao ya ndani kutekeleza shughuri mbalimbali.”Amesema Fidea

Pia ameelezea mafanikio waliyoyapata kama mashirika kwa ujumla ni utekelezaji wa miradi 76 yenye thamani ya shilingi bilioni 11 na kuwafikia wananchi zaidi ya 500,000 katika miradi hiyo na kuahidi kuendelea kuongeza juhudi ya kutafuta rasilimali ili waweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani John Samo amesema kutokana na changamoto kubwa ya mashirika kutegemea ufadhili sheria imeleta mabadiliko ambayo taasisi inaruhusiwa kufanya biashara na faida inayopatikana iwasaidie kutekeleza miradi katika jamii na ametoa wito kwa mashirika kubadilisha fikra ya kudhani kuwa utekelezaji wa mradi ni lazima kusubiri fedha kutoka kwa wafadhili wa ndani au nje ya nchi na badala yake wafikilie kuanzisha miradi itayowasaidia.

Akizungumza kwa niaba ya Mku wa Wilaya ya Mtwara Mwanamtama Pole ambae ni Afisa Tarafa wa Mikindani ametoa wito kwa baadhi ya mashirika yanayojihusisha na masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia kuhakikisha wanayafikia makundi yote hususani watoto wa kiume ambao wapo katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukatili kutokana na kusahauliwa.

Wilaya ya Mtwara ina jumla ya Mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali 42 yakitekeleza afua mbalimbali kama vile elimu, afya,kilimo,maji, mazingira,jinsia na gesi asilia lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali kuwaletea maendeleo wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!