Latest Posts

PM MAJALIWA ATAKA USALAMA WA TAARIFA ZA WATUMISHI UZINGATIWE

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amehitimisha kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na kuzindua mifumo ya kidijiti iliyosanifiwa na kujengwa na wataalamu wa ndani huku akisisitiza kuzingatiwa usalama wa taarifa za watumishi wa umma ili kuepuka uhalifu wa mtandao.

PM Majaliwa ametoa maagizo hayo Jumapili Juni 23, 2024 Jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha kilele hicho na kusema kuwa mfumo utawabana watumishi wazembe.

“Ninaagiza taasisi kuimarisha mifumo na miongozo ili itumike kwa uaminifu, taasisi kutoa mafunzo kwa watumishi juu ya namna ya kutumia mfumo, pia taasisi zinatakiwa kuwa na mfumo wa ufuatiliaji na tathimini ili kufuatilia viashiria vya utendaji” Amesema Majaliwa.

Mifumo hiyo ambayo imeelezwa kuwa italeta mageuzi makubwa katika utoaji huduma kwa wananchi itajulikana kama ‘E Watumishi’ ikitarajiwa kujumuisha mifumo jumuishi ya taarifa na mshahara, mfumo wa usimamizi na utendaji kazi, mfumo wa tathimini na E Mrejesho.

Hata hivyo amefafanua kuwa kila taasisi inatakiwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo sekta binafsi ili mfumo ulete manufaa kwa wote, pamoja na kujiunga na kutumia E Utumishi na kuweka ukomo kwa taasisi za umma kujiunga na mfumo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo wezeshi ya utoaji huduma kwa wananchi na kuondoa kero ikiwamo rushwa. Amesema kuwa mifumo hiyo itaondoa upendeleo wa utendaji kazi wa watumishi, na taasisi zinaweza kufuatiliana.

Amesema kuwa zoezi la kuwabaini watumishi limefanyika katika taasisi 571 na litaendelea kufanyika kwa msawazo wa watumishi, na kudai  mifumo hiyo inasomana na kubadilishana taarifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!