Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametembelea mazoezi ya timu ya soka ya Biashara United Mara kisha kuzungumza na wachezaji kuelekea mchezo wa Play Off ya Kwanza utakaopigwa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume dhidi ya Tabora United.
Akizungumza na wachezaji Mtambi amesema ni wakati wa Wanamara kurejea ligi kuu hivyo washikamane na kuweka tofauti pembeni na amewataka Wanamara kuujaza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma ili kutoa hamasa kwa wachezaji.
Kwa upande wake kocha Mkuu wa klabu ya Biashara United Aman Josiah amekiri kuwa mechi yao dhidi ya Biashara United itakuwa ngumu kutokana na ubora wa timu ya Tabora hata hivyo kupitia ugumu huo wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo utakaopigwa Jumatano Juni 12.
Aidha mchezaji kiongozi wa Biashara Babilas Chitembe amesema wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo wa Jumatano.