Latest Posts

RIPOTI: TANZANIA YATAJWA MIONGONI MWA MATAIFA 10 BORA AFRIKA KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Utamaduni wa matengenezo ya barabara barani Afrika ni suala lenye changamoto nyingi na linahitaji juhudi za ziada. Wakati baadhi ya nchi za Afrika zikipiga hatua kubwa katika kuendeleza na kudumisha miundombinu ya barabara, nchi nyingine bado zinakabiliwa na changamoto za miundombinu hafifu, ukosefu wa matengenezo ya mara kwa mara, na uhaba wa uwekezaji kwenye mifumo ya usafirishaji.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Statista iliyochapishwa na Businessinsider mwishoni mwa Oktoba 2024, Tanzania imeorodheshwa kama moja ya nchi 10 bora barani Afrika zenye miundombinu bora ya barabara.

Tanzania imechukua nafasi ya tisa kati ya nchi kumi, ikipata alama 4.41. Nafasi ya kwanza katika orodha hiyo inashikiliwa na Namibia yenye alama 5.57, ikifuatiwa na Misri (5.53), Benin (5.0), na Rwanda (4.86). Nchi nyingine zilizoorodheshwa ni pamoja na Mauritius, Ivory Coast, Morocco, Kenya, na Afrika Kusini ambayo inashika nafasi ya kumi kwa alama 3.97.

Ripoti hii inakuja wakati ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara, kuanzia maeneo ya mijini hadi vijijini.

Uwekezaji huu mkubwa unalenga kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa, hivyo kuwawezesha wananchi kushiriki kwa urahisi katika shughuli za kiuchumi na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kwa kuweka mkazo kwenye miundombinu, Tanzania inaonyesha dhamira ya kuimarisha uchumi kupitia barabara bora ambazo zinasaidia kupunguza gharama za usafirishaji, kuongeza fursa za biashara, na kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida. Serikali inategemea kuwa juhudi hizi zitawezesha Taifa kuendelea kufikia malengo yake ya maendeleo endelevu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!