Latest Posts

SHIRIKA LA YAPPO LAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KWA KUTOA MSAADA SHULE YA MSINGI TANGAZO

Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala mbalimbali ya maendeleo ya jamii la Youth And Planet Protectors Organization (YAPPO) limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kwenye shule ya msingi Tangazo iliyopo kata ya Tangazo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa Februari 10, 2025 shuleni hapo ikiwemo Mashine ya kudurufia mitihani (photocopy machine),Tanki la maji lenye ujazo wa mita 300 pamoja na mipira .

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mhasibu wa Shirika hilo la YAPPO Hamisi Mwarabu amesema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure.

Aidha vifaa hivyo vitakwenda kuwarahisishia walimu kwenye kuandaa mitihani pamoja na kuhifadhi maji sehemu salama.

Akizungumzia manufaa watakayoyapata kutokana na uwepo wa vifaa hivyo shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tangazo Abdallah Salumu amesema ni kuongeza kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.

Amesema kabla ya mashine hiyo wanafunzi hao walikuwa wanafanya mitihani kwa uchache kutokana na gharama za maandalizi ya mitihani hiyo.

Nae Diwani wa kata ya Tangazo Mohamedi Muwanya metoa wito kwa walimu shuleni hapo kutunza vifaa hivyo hususani mashine ili iweze kuwasaidia kwa siku nyingi zaidi kutokana ilikuwa ni kilio chao kikubwa kwa siku nyingi.

Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo ikiwemo Faudhia Omari “Nalishukuru shirika hili la YAPPO kwa msaada huu mkubwa waliowapatia na  tunaahidi kufanya mitihani ya majaribio kwa kadri walimu watavyoiandaa na kutunza vifaa vyote tulivyoletewa”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!