Latest Posts

HAPI AKUTANA NA RAIS WA MSUMBIJI, AWASILISHA SALAMU ZA MWENYEKITI WA CCM DKT. SAMIA

Katibu Mkuu wa Wazazi Comrade Ally Salum Hapi amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji ambaye pia ni Rais wa Chama tawala cha FRELIMO nchini humo Mhe. Daniel Francisco Chapo.

Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Chimoio, Msumbiji, tarehe 22 Agosti 2026 wakati Hapi akimuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro kwenye Kongamano la 11 la kitaifa la Makada wa FRELIMO linaloongozwa na Rais Daniel Francisco Chapo, ikiwa ni hatua ya kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama tawala cha FRELIMO utakaofanyika mwakani 2027.

Katika mazungumzo hayo, Comrade Hapi amewasilisha salamu za kheri, udugu na ushirikiano kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Chama Cha Mapinduzi na FRELIMO vina uhusiano wa kihistoria na wa kidugu uliodumu tangu wakati wa harakati za ukombozi wa mataifa hayo mawili.

Chama cha FRELIMO kilizaliwa jijini Dar es salaam, Tanzania tarehe 25/06/1962.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!