Latest Posts

SHUGHULI ZA UVUVI KUSIMAMISHWA KWA MUDA MWALO WA MAKATANI

 

Timu ya Menejimenti kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita ,imefanya ziara katika mwalo wa Makatani Kata ya Nkome ili kuona hatua ambazo zilitolewa na uongozi wa Halmashauri mapema May 4,2024 za Wananchi hao kuondoka katika eneo la mwalo huo iwapo zimetekelezwa kutokana na kujaa kwa maji ya Ziwa Viktoria tokea May 2, 2024.

Akizungumza katika eneo la Kata ya Nkome, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Modest Buchard amesema iwapo magonjwa ya mlipuko yataibuka hayachagui mtu wa kumpata. ” Tumeona hali sio nzuri hivyo tumeona Shughuli za Uvuvi zihamishiwe sehemu zisiendelee ili uwepo urahisi wa kuwaondoa watu. ‘ “Tutasimamisha shughuli z Uvuvi ili watu waeze kupisha eneo hilo kuepuka magonjwa ya mlipuko. Shughuli zisiendelee kwa muda ili vibanda hivyo vihamishwe.” Amesema Dkt Modest

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Nkome ndugu Festo Nsalamba amesema swala la kuhamisha vibanda sio rahisi ila litatekelezwa kama ilivyo agiza Ofisi ya Mkurugenzi na kuomba ofisi ya Mkurugenzi iwezeshe gari la matangazo ili kurahisisha matangazo kwani nyakati za Asubuhi watu wanaofika katika mwalo huo ni zaidi ya watu elfu tano.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihumilo ambapo mwalo wa Makatani upo, ndugu Tumaini Christopher amesema tukio hilo lilianza tarehe 2 May, 2024 na wengi wa wakazi katika eneo hilo hawana makazi ya kudumu hivyo wanaweza kuondolewa kwani wameyafuata maji kwa kujenga vibanda na kusema huduma za kijamii zisimamishwe na watashirikiana na uongozi wa Serikali ili kuepuka madhara ya kiafya ambayo yanaweza kutokea kutokana na hali ya uchafu katika eneo hilo

Kwa upande Mwingine,
Msimamizi wa Shughuli za Uvuvi ndani ya ufukwe wa ziwa Viktoria katika mwalo wa Makatani ndugu Baraka Pantaleo amesema eneo kubwa limevamiwa na maji na kusema watu wameanza kutoka kwa hiyari na baada ya kuwatangazia kuondoka katika eneo hilo na pia amebainisha mara baada ya zoezi la kuhama kukamilika usafi utafanyika ili Shughuli za Uvuvi ziweze kuendelea kama awali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa eneo hilo wamesema wamenza kuondoka eneo hilo kama agizo lilivyotolewa ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!