Latest Posts

SOKO KUU MTWARA WALIA NA MIUNDOMBINU MIBOVU YA CHOO

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu lililopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wamelalamikia kukosekana kwa huduma ya choo katika soko hilo hali inayopelekea kufuata huduma hiyo kwa wakazi wa maeneo jirani na soko hilo.

Hayo wameyaeleza Novemba 19, 2024 kwenye ziara ya Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Mtenga ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ukarabati wa soko hilo ambapo wafanyabiashara hao wamesema kukosekana kwa huduma muhimu hiyo kunahatarisha afya zao.

Mwanahamisi Mlaponi ni miongoni mwa wafanyabiashara katika soko hilo, amesema huduma ya choo wanaipata kwa majirani waliopo karibu na soko hilo kutokana na kufungwa kwa choo ambacho hapo awali walikuwa wanatumia hivyo ameiomba serikali kuwajengea choo pamoja na kuwawekea huduma ya maji.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko Kuu Mtwara (WABISOKO) Mshamu Kaisi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo pia inakosesha mapato ya kutokana na wafanyabiashara hao kufuata huduma hiyo maeneo jirani.

“Majirani hao wametumia fursa hiyo kutengeneza vyoo vya biashara na kusababisha wafanyabiashara kuacha biashara zao na kutumia mda mrefu kwa ajili ya kuifuata huduma ya hiyo ya choo”Amesema Kaisi.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mwalimu Hassan Nyange amesema hali hiyo imesababishwa na ukuaji wa mji inayopelekea ongezeko kubwa la watu hivyo tayari wameanza ukarabati wa choo katika soko hilo kwani zaidi ya Shilingi milioni 20 imetolewa kwa ajili ya ukarabati wa choo.

Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Mtenga amemsisitizia mkurugenzi huyo kuona namna ya kuharakisha ukarabati huo ili kuondoa usumbufu unaowakumba wafanyabiashara hao kutokana na umuhimu wa huduma ya choo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!