Latest Posts

SPIKA TULIA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA KWA UMAHIRI WA UTENDAJI

Na Theophilida Felician.

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Tulia Ackson, amepongezwa kwa utendaji wake mahiri na uwajibikaji tangu aliposhika nyadhifa hizo.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa Taasisi ya International Peace Information (I.P.I), Prof. Wilson George Munguza, alipokuwa akizungumza katika makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo Temeke, Dar es Salaam. Prof. Munguza amesema wao kama wadau wa maendeleo kupitia juhudi za kuhamasisha utunzaji wa amani, waliguswa na uongozi wa Spika Tulia, hivyo wakaamua kumtunuku tuzo ya heshima.

Prof. Munguza amesema hivi karibuni timu ya wanataasisi wapatao 200 kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Visiwani, pamoja na wenzao kutoka Uganda, walifika Bungeni jijini Dodoma kumkabidhi rasmi tuzo hiyo Spika Tulia.

Ameeleza kuwa hatua hiyo ilichochewa na kutambua jinsi Tulia alivyojidhihirisha kuwa kiongozi mchapakazi tangu alipoanza majukumu yake ya kibunge, na sasa anaipeperusha vyema bendera ya nchi kupitia nafasi yake katika Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Ametaja kuwa uongozi wake ni mfano wa kuigwa.

Aidha, Prof. Munguza amewashukuru wanataasisi wenzake kwa mshikamano na kujitoa kwao kuhakikisha tukio hilo linafanikiwa, na ameahidi kuwa taasisi yao itaendelea kutambua na kuthamini viongozi wanaoleta mabadiliko chanya katika jamii kama Tulia Ackson.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!