Latest Posts

TANZANIA YAANZA KUTEKELEZA MPANGO WA KUVUTIA MITAJI KUTOKA CHINA

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeanza kutekeleza mpango maalum wa kuvutia mitaji ya uwekezaji kutoka China ili kuhakikisha uwekezaji kutoka China unaongezeka. Mpango huo ni matokeo ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa FOCAC nchini China.

Katika mkutano huo Rais wa Jamhuri ya China, Xi Jinping aliahidi kiasi cha Dola bilioni 10 kuwekezwa Afrika kupitia mpango maalumu wa kukuza uwekezaji Afrika.

Kutokana na ahadi hiyo ya Rais wa China kuwekeza mitaji Afrika, Waziri wa Mipango na Uwekezaji Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo aliiagiza TIC kuwa na mkakati wa kuhakikisha angalau theluthi moja ya mitaji hiyo ambayo ni Dola bilioni tatu inawekezwa Tanzania kutoka China.

Ni kutokana na dhamira ya utekelezaji wa agizo hilo, TIC imezindua kituo cha kuvutia uwekezaji nchini China katika Jimbo la Hunan ambalo limeteuliwa kuwa lango la uwekezaji kutoka China ili kuhamasisha na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na kuleta mitaji ya uwekezaji Tanzania kutoka China. Jukwaa hili limezinduliwa na Kaimu Konseli Mkuu, Ali Mohamed Mwinyi, anayesimamia Ubalozi mdogo wa Tanzania nchini China.

Akiongea katika tukio hilo ambalo lilikutanisha kampuni zaidi ya 150 kutoka sekta mbalimbali nchini China, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri amesema jukwaa hilo ni mwanzo wa utekelezaji wa mpango wa kuvuta uwekezaji kutoka China, ikitarajiwa ongezeko la wawekezaji wengi kutoka China kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Viongozi hao baada ya uzinduzi walipata fursa ya kutembelea viwanda vikubwa nchini China kwa lengo la kuvishawishi kufanya uzalishaji kupitia Tanzania

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!