Latest Posts

TATA YAJA NA SULUHISHO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI NCHINI

Kampuni ya magari ya TATA Tanzania imezindua mpango maalum kwa ajili ya sekta ya usafirishaji wa mizigo mikubwa nchini kwa kuzindua trela za mizigo aina ya ‘Tiva Trela’ ili kumrahisishia mfanyabiashara na mkulima kupakia mizigo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo na Masoko, Smart Deus amesema  lengo  la mpango huo ni kuwaweka karibu wateja na kampuni katika  msimu  huu wa mauzo  na mavuno nchini ambapo magari hayo yanapatikana kwa mkopo pia.

“Uzinduzi huu umeambatana na utambulisho wa trela ya kubebea mizigo mikubwa kwa wakati mmoja. Pia tumeandaa mpango maalumu kwa wateja watakaowahi kipindi hiki cha mwanzo kuna mikopo isiyo na riba na ile ambayo dhamana ni kifaa usika kwa kushirikiana na tasisi za fedha kuelekea msimu wa mauzo na mavuno,” amesema.

Pia amefafanua kuwa wana mpango wa kuzunguka nchi mzima ili kuwafikia wateja wakitambua kuwa siyo kila mteja atafuata bidhaa Dar es Salaam, hivyo kupitia matawi yake yaliyopo maeneo yote nchini basi mteja atahudumiwa.

Ameeleza kuwa kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 (kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan) kumekuwa na wakati mzuri kibiashara kutokana na milango ya biashara kufunguka. Ameongeza kuwa wameahidi kushirikiana na serikali na wadau wao kwa kuleta bidhaa bora zaidi zinazokidhi mahitaji ya Watanzania.

Amesema kwa zaidi ya miaka 20 ya kampuni hiyo nchini, wamebaini uwepo wa changamoto katika usafirishaji kulingana na mazingira na barabara, hivyo wakaamua kuja na suluhisho la kuleta magari yenye uwezo wa kuendana na mazingira hayo.

Naye Meneja Mauzo wa TATA, Kitengo cha Force Motors, Robert Mwakabibi amesema mapinduzi hayo hayajaacha nyuma usafirishaji wa abiria kwani walileta gari salama ili kupunguza adha ya usafiri na kuwaongezea kipato wamiliki na madereva wa daladala.

Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya TATA ,Smart Deus (kulia) akizungumza wakati wa Uzinduzi Trela za mizigo  mikubwa aina ya TIVA  jijini Dar es salaam

Aidha amesema kwamba mapinduzi hayo hayajaiacha sekta ya elimu, kwani magari salama yaliyoletwa yanawagusa wanafunzi moja kwa moja baada ya kubaini magari mengi ya shule hayajatengenezwa katika mfumo mzuri.

“Ukiangali gari zetu ni tofauti na nyingine, gari nyingi zinaletwa zikiwa zina muda mrefu lakini za kwetu ni kipindi hiki hiki zinapoingia.  Gari za shule nyingi zilizopo hazijatengezwa maalum kwa ajili ya wanafunzi lakini za kwetu zina mfumo wa kuhudumia wanafunzi wa aina zote, wa kawaida na wenye mahitaji maaalum”, ameeleza na kuongeza,

“Tumeona soko linauhitaji mkubwa kwa usafiri wa wanafunzi, taasisi za serikali na binafsi”.

Amesema wameweka mfumo mzuri wa mteja kupata gari hizo ambapo kuna kulipa fedha taslimu, na mkopo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha. Akizungumzia jinsi mkopo wa magari hayo unavyotolewa, Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Begumisa Egbert, amesema mkopo usio na riba mteja anatakiwa kulipa asilimia 50 na nyingine iliyobaki inalipwa kwa kipindi cha miezi 12.

Ameeleza kuwa mkopo mwingine ambao utakuwa na riba kidogo, mteja anatakiwa kulipa asilimia 20 ya bei ya gari anayotaka, kisha iliyobaki inalipwa kwa kuanzia miezi sita mpaka miaka mitatu.

TATA ni wauzaji pekee nchini Tanzania wanaouza gari za mizigo, abiria na za kibiashara. Ili kumfikia kila mmoja, siku za usoni TATA watakuwa na kampeni ya Twende Pamoja na TATA, kuhakikisha kila mmoja anapata huduma mpaka barazani kwake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!