Latest Posts

TBS YATAHADHARISHA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU

Na Vivian Ricardo,

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeonya wananchi kuhusu matumizi ya vipodozi visivyo salama, likisema bidhaa hizo zinaweza kusababisha madhara makubwa kiafya, ikiwemo magonjwa sugu kama saratani.

Onyo hilo limetolewa na Meneja wa Ukaguzi na Uzingatiaji wa Sheria wa TBS, Nuru Mwasulama, ambaye amesema shirika hilo linaendelea kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa vipodozi vinavyouzwa nchini.

Nuru mwasulama ametoa wito kwa wauzaji wa vipodozi kuuza bidhaa hizo katika maeneo ambayo yamesajiliwa, ili kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa hizo.

“Tumekuwa tukikutana na bidhaa za dawa za cheti kwenye maduka ya vipodozi zikiuzwa kama vipodozi. Hilo ni kosa kisheria kwani inaweza kupelekea usugu wa dawa, hali ambayo inaweza kuathiri uwezo wa dawa hizo kutibu mgonjwa atakapohitaji matibabu baadaye”, amesema Nuru.

Amewakumbusha pia si salama kuuza vipodozi vilivyokwisha muda wa matumizi pamoja na bidhaa zenye viambata sumu, ambavyo tayari vimepigwa marufuku kutumika kwani ni hatari kwa afya kwa sababu ngozi inaweza kuruhusu baadhi ya kemikali kuingia mwilini.

TBS pia imekuwa ikifuatilia matangazo ya vipodozi kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kubaini ongezeko la maudhui yanayopotosha wananchi kuhusu matumizi na utengenezaji wa bidhaa hizo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!