Latest Posts

UNYANYASAJI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII NI KIKWAZO KATIKA UTELEZAJI WA MAJUKUMU

Wanawake wanaojihusisha na utetezi wa haki za binadamu kupitia majukwaa ya kidijitali wameitaja changamoto ya udhalilishaji kwenye mitandao ya kijamii (cyberbullying) kuwa miongoni mwa vikwazo vinavyowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kutetea haki za binadamu mtandaoni.

Hayo yameelezwa na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo uliandaliwa mjadala maalumu uliowakutanisha wanawake wanaojihusisha na utetezi wa haki za binadamu kidijitali kwa lengo la kutathmini hali ya utetezi wa haki hizo katika mazingira ya mtandaoni pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanapotekeleza majukumu yao

Mjadala huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Miradi na Uendeshaji wa THRDC, Wakili Halima Sonda, na ulihusisha washiriki kutoka sekta mbalimbali wanaotumia majukwaa ya kidijitali kuhamasisha na kutetea haki za binadamu.

Akizungumzia changamoto ya udhalilishaji mtandaoni, Dkt. Kuduishe Kisowile ambaye ni daktari na mtetezi wa haki za binadamu mtandaoni alisema wanawake wengi wanaojitokeza kuzungumzia masuala ya haki hukumbana na lugha chafu, kejeli na mashambulizi ya maneno yanayolenga kuwavunja moyo.

Hata hivyo aliwahimiza watetezi wa haki za binadamu kutochukulia kwa uzito maneno ya dharau yanayotolewa mitandaoni ili yasiwakatisha tamaa.

Kwa upande wake, Wakili Janeth Kahindi alisema ingawa zipo sheria zinazosimamia masuala ya udhalilishaji mtandaoni, bado changamoto ipo katika utekelezaji wake. Alieleza kuwa watu wengi hushindwa kufungua mashauri mahakamani kutokana na ugumu wa kukusanya ushahidi wa kidijitali na taratibu za kisheria zinazoweza kuwa ndefu.

Naye mtangazaji Najma Paul alisema hata ndani ya tasnia ya habari bado kuna changamoto kwa wanawake kuaminiwa katika majukwaa ya maamuzi, ambapo mara nyingi uwezo wa wanaume huaminiwa zaidi kuliko wa wanawake.

Washiriki wa mjadala huo walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi kwa watetezi wa haki za binadamu mtandaoni pamoja na kuongeza elimu kuhusu matumizi salama ya majukwaa ya kidijitali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!