Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeendelea na utekelezaji wa miradi ya uhifadhi wa mazingira ikiwemo mradi wa ufugaji wa samaki kwa lengo la kuishirikisha moja kwa moja jamii katika uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kuwapatia shughuli mbadala za kufanya pasipo kuathiri mazingira.
Akizungumza katika zoezi la uvunaji wa samaki lililofanyika katika Kijiji cha Msonge Mkoani Morogoro, Mhandisi Paschal Joseph ambaye ni Afisa Kidakio cha Ruvu amebaisha kuwa walianza na utoaji wa elimu kwa wananchi na kisha kuwasajili katika vikundi na kuwawezesha miradi ya ufugaji w samaki ili waachane na shuguli za uharibifu wa mazingira
Nao baadhi ya wananchi wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kuwezesha kuwapatia miradi hiyo huku wakiahidi kuendelea kutunza mazingira hususani vyanzo vya maji.
