Latest Posts

News, Njombe.

Mbunge wa Jimbo la Lupembe Wilayani Njombe Edwin Swalle amewaagiza wazee kwenda kuzungumza na mwananchi aliyefahamika kwa jina la Ngewe anayedaiwa kuzuia nguzo za umeme wa REA kupita kwenye shamba lake na kusababisha wananchi wengine kukosa umeme kutokana na zoezi hilo kusimama huku yeye akiwa ameshapata umeme.

Swalle ametoa agizo hilo kwa wazee wa kijiji cha Image wakati akizindua ofisi mpya na ya kisasa ya kijiji hicho iliyokamilika kwa kujengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 56 ambapo amesema wataalamu wanataka kuendelea na kazi ya usambazaji wa umeme lakini zoezi hilo limekuwa likikwamishwa na baadhi ya watu wachache.

“Mradi wa umeme ukipita kwenye maeneo yenu hauna fidia na unapokuja kwako ujue umepita kwa watu wengine, sasa nimesikia kuna wananchi wamezuia umeme usipite kwenye mashamba yao, hao ni wapinzani wa maendeleo ya nchi yetu, wazee si mpo hapa?  Mkamwambie Ngewe basi aruhusu umeme upite maana kwake umefika ukitoka kwenye mashamba ya wenzake, jambo hili ninawaachia wazee” Ameeleza Swalle.

Nao baadhi ya wazee akiwamo Japhari Kitago na Agnes Kuchungulwa wamesema wamepokea agizo la mbunge la kwenda kukaa na Ngewe ambapo nao pia wamemtaka ndugu yao kukubali umeme kupita.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!