News, Njombe.
Kijana Shadrack Utungulu mkazi wa kijiji cha Igominyi kata ya Yakobi halmashauri ya mji wa Njombe amejikuta matatani mara baada ya kukutwa akimshika chuchu na mkia ng’ombe asiye wake, na kuingia kwenye kashfa nzito ya kunajisi mnyama huyo.
Tukio hili linajiri wakati ambao kuna maelezo ya kijana huyo kuwa na historia kama hiyo hapo awali, ambapo alikutwa na tuhuma ya kunajisi ng’ombe, lakini aliweza kutafuta suluhu na mmiliki baada ya mama yake kulipa ng’ombe mwingine.
Faustine Mdendemi ni mmiliki wa ng’ombe aliyekuwa akishikwashikwa, anasema siku ya tukio alikuwa akitoka nyumbani kuelekea shambani na kumkuta akiwa kwenye zizi la ng’ombe.
“Nikamuuliza unafanya nini ndani? Nilijibiwa kwamba ninaomba tumalizane, nilivyomkamia alitoka bandani akanipiga kichwa na kuanza kunigalagaza chini huku akinikaba shingoni, nilivyokuta naelemewa nilisema yameisha niache, baada ya mimi kusema hivyo aliniachia nikapiga ‘ngolo’ ndipo watu wakaja kunisaidia”, amesema Mdendemi.
Baadhi ya wananchi na wafugaji wa Igominyi wanasema kitendo kilichofanywa na kijana huyo kinawapa wasiwasi mkubwa kwa kuwa ana akili timamu lakini wanashangaa anayoyafanya huku wakihofia zaidi watoto wao kubakwa.
Thelesina Manga ni mtendaji wa kijiji cha Igominyi, anasema baada ya kumkamata kijana huyo, hatua inayofuata ni kumfikisha kituo cha polisi kwa kuwa jambo hilo lipo juu ya uwezo wake
“Hatua ninayochukua kwasababu lipo juu ya uwezo wangu mimi, ninampeleka Polisi kwa ajili ya hatua zaidi, wenzetu waende kufanya uchunguzi”, amesema Thelesina Manga.