Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa,Mary Pius Chatanda amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili jumuiya hiyo imekuwa ikiandaa mafunzo kwa viongozi wake kuanzia ngazi ya matawi, kata,wilaya na mikoa pamoja na watumishi wake yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu katika nyanja za kisiasa, wlimu, kiafya pamoja na mtumizi ya nishati safi.
Mwenyekiti Chatanda ameeleza hayo leo Septemba 26, 2024 wakati wa ufunguaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika wilaya ya Songea mjini mkoani Ruvuma.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili yakifuatiwa na Kikao cha Baraza Kuu la UWT kitakachonyika tarehe 28 Septemba, 2024 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.