Latest Posts

DC MBEYA APOKEA SARUJI, SAMANI UBORESHAJI ELIMU

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa, amepokea mifuko 200 ya saruji kutoka kiwanda cha saruji Mbeya kwa ajili ya shule ya Sekondari Usongwe ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula unaoendelea kujengwa shuleni mjini Mbalizi.

Pamoja na mchango huo wa wadau, mkuu huyo pia amepokea viti na meza 220 kwa ajili ya shule ya Sekondari Songwe vilivyotolewa na Kampuni ya Saruji (Mbeya cement).

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno M. Malisa amekabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa shule hizo mbili za sekondari na kuwasisitiza utunzaji wa viti na meza ili viweze kutumika kwa muda mrefu.

Pia amewataka wazazi kuendelea kuwahimiza watoto wao kusoma ikiwemo kuwapeleka shule watoto wote ambao wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2025 na bado hawajaripoti shuleni.

“Mtoto ili aweze kusoma vizuri, anatakiwa kuwa ameshiba hivyo ni wajibu wetu wazazi na walezi kuchangia chakula shuleni lakini pia tuhakikishe watoto wote waliochaguliwa kujiunga na sekondari waende kwani Serikali imeweka mazingira sawa kwenye shule zetu na ninyi wanafunzi hakikisheni mnasoma kwa bidii”, ameeleza DC Malisa.

Diwani wa kata ya Bonde la Songwe Michael Ngailo, amewashukuru wadau hao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha miundombinu katika shule yake ya sekondari na kwamba wamekuwa wakishirikiana nao katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kilichofanywa na kiwanda cha Saruji (Mbeya Cement) ni kuunga mkono jitihada za Serikali na wadau wengine katika kuboresha miundombinu hasa kwenye sekta ya Elimu hapa nchini katika kuhakikisha watoto wanasoma na kujifunzia kwenye mazingira rafiki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!