Latest Posts

MADIWANI MVOMERO WATAKA UFUMBUZI WA KUDUMU MIGOGORO YA WAKULIMA

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero wakiongozwa na Amini Membe, Diwani wa Kata ya Melela, pamoja na Elimu Kisugulu, Diwani wa Kata ya Doma, wameomba hatua zaidi zichukuliwe kunusuru wakulima wanaoathiriwa na wafugaji wanaoingiza mifugo katika mashamba yao.

Wametoa kauli hiyo leo Agosti 27, 2026, wakati wa Kikao cha Mabaraza ya Madiwani, wakieleza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwaletea hasara wakulima na kufifisha jitihada za kampeni ya “Tutunzane”, iliyolenga kuwa sehemu ya suluhisho la migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Madiwani hao wamesisitiza umuhimu wa mamlaka husika kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa sheria ili kulinda maslahi ya wakulima, huku wakitaka hatua madhubuti zichukuliwe ili migogoro hiyo ipatiwe ufumbuzi wa kudumu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Maulid Dotto, amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama imekuja na mkakati mpya unaolenga kuweka makubaliano yatakayowawezesha wafugaji kufuga kwa kuzingatia utaratibu na kutumia njia za kisasa za ufugaji.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!