Latest Posts

HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA YALENGA KUKUSANYA BILIONI 13, YAJIVUNIA REKODI YA KUPATA HATI SAFI

Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa, Ibrahimu Ngwada, amesema halmashauri hiyo tangu ichukuliwe kutoka CHADEMA mwaka 2020 hadi sasa imekuwa ikipata hati safi za ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Ngwada ameyasema hayo leo, Agosti 27, 2026 katika Baraza la Madiwani la mwisho lililokuwa na jukumu la kupitia na kujadili hesabu za mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2026.

Amesema wakati walipopokea Halmashauri hiyo, makusanyo ya mapato yalikuwa takribani Sh bilioni 4 pekee, lakini kwa sasa Halmashauri inakusanya zaidi ya Sh bilioni 11, katika bajeti ya sasa wanapanga kukusanya Sh bilioni 13.

Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020, Halmashauri hiyo ilikuwa ikiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo Alex Kimbe alikuwa Meya, kuanzia mwaka 2020 hadi sasa, uongozi wa halmashauri hiyo umechukuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!