Latest Posts

“MAADILI MEMA NI MSINGI WA UTU, UMOJA NA MSHIKAMANO WA TAIFA”

 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inaendelea na shamrashamra za Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni, huku siku ya pili ya tamasha hilo ikiambatana na ufunguzi rasmi pamoja na Mdahalo wa Kitaifa kuhusu maadili uliojadili namna ya kuhamasisha na kuchochea maadili mema kwa Watanzania.

Mdahalo huo umefanyika Agosti 26, 2026, katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), ambapo wataalamu na wadau wa maadili wameeleza umuhimu wa jamii kuzingatia maadili katika maisha ya kila siku.

Watoa mada wamesisitiza kuwa tunapokuwa na kiu ya jamii yenye maadili, tunapaswa kuwa mfano bora kwa kuonesha mwenendo unaojenga jamii na kuhakikisha tunawaongoza wengine kupitia matendo yetu mema.

Aidha, imeelezwa kuwa maadili ni msingi wa utu, umoja na mshikamano wa taifa, hivyo Watanzania wanapaswa kuwa mfano bora kwa watoto na jamii kwa ujumla, kuipenda Tanzania kwa vitendo, kuheshimu utu wa wengine na kujenga taifa lenye amani, umoja na mshikamano.

Wadau hao wameeleza kuwa maadili mema ni utambulisho wa Mtanzania na yanapaswa kuenziwa na kuendelezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!