Latest Posts

JESHI LA POLISI LAENDELEA KUTAMBUA JITIHADA ZA ASKARI WANAWAKE KATIKA KUDHIBITI UHALIFU.

Askari wanawake kutoka Jeshi la Polisi nchini, wameendelea kuungwa mkono kutokana na jitihada zao mbalimbali katika kudhibiti vitendo vya uhalifu ikiwemo makosa yanayotokana na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 24, 2026, jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF Net), Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Kheriyangu Khamis, wakati akizungumza na askari wanawake, maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na Vikosi mbalimbali.

DCP Kheriyangu amesema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, ambapo alisema jitihada hizo zinapaswa kuendelezwa na askari wanawake kwa kuongeza juhudi na maarifa katika kutekeleza majukumu yao, hususani kutoa elimu kwa jamii kuhusu Kubaini kutanzua na kudhibiti uhalifu.

Aidha, amewataka askari wanawake kuendelea kushirikiana kupitia mtandao wao na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa uadilifu, weledi na uzalendo, kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!