Latest Posts

‎KANISA LACHANGIWA 75,805,000,GENERAL WAITARA ACHANGIA 17,500,000

Na Helena Magabe -Tarime

‎Kanisa la  Roman Katoliki parokia ya Kyeisangora Nyamwaga Tarime limechangiwa shilingi 75,805,000  pamoka na mifuko 20 ya saruji katika harambee  ili  kuendeleza ujenzi wa kanisa jipya linalojengwa katika parokia hiyo.

‎Katika harambee hiyo iliyofanyika juni 29,2025  alikuwa Mgeni rasmi alikuwa Simon Mseti  Mkurugenzi wa Goldland Hotel iliyopo Tarime alichangia 14,400,000 ambapo aliendelea kufanya harambee huku waumini wakiendelea kuchangia na wengine wakituma pesa kwa Paroko wa Parokia hiyo Padri Julius Manyonyi na wengine wakiwasilisha slip za Benki na hatimaye zikafika 75,805,000 .

‎Mkuu wa Majeshi mstaafu George waitara alichangia 15,000,000 huku wadogo zake Wawili wakiunga kwa 2,500,000 ,Anita Waitara 2,000,000 ,Amos Waitara 500,000 hivyo Familia ya Waitara jumla ilichangia 17,500,000 lakini pia Familia ya Padri Manyonyi nayo ilichangia 1,300,000 kwa kuunga juhudi za ndugu yao katika ujenzi wa kanisa hilo michango mingine ilichangwa toka latika vigango 10 vya parokia hiyo na mingine ilitoka katika baadhi ya  makanisa pamoja na wadau mbali mbali wakiwemo marafiki wa Mseti.

‎Padri Cleophace Sabure ambaye alimwakilisha   Mhashamu Askofu wa jimbo la Musoma  Michael Msonganzila alisema kuwa ,Askofu hakutaja kiasi atachachochangia isipokuwa alimwambia ataongea na Padri Manyonyi ili kuangalia nini cha kufanya na kuongeza kuwa jimbo lina parokia 43,shule za msingi 39 ,shule za sekondari 7 Chief wanzagi,Kowak Girls,Nyegina,St Alberto,Masonga,Little Flower pamoja na Makoko Seminary ambapo  Msamamizi ni  Askofu Msonganzila.

‎Alisema alimwambia baada ya kupata mwaliko wa harambee aliomba ili Mungu awaguse watu mbali mbali waweze kuchangia na kuongeza kuwa Askofu alisema katika michango ya Kanisa kuna vitu vitatu Sara,hali pamoja na mali na alisema kanisa litajengwa na waumini hata bila kutegemea misaada ya nje hata hivyo Padri Sabure ambaye ni Paroko wa Parokia ya Kowak alichangia 300,000 .

‎” Baba Askofu amesema kwenye michango ya kanisa kuna vitu vitatu ambavyo ni sala,hali na mali amesema kanisa litajengwa na waumini tukitegemea misaada toka nje inachelewa unaweza kuomba milioni 10,000,000 ukakaa hata miaka miaka miwili” alisema Padri Sabure

‎Amos Waitara ambaye alikuwa  Mshereheshaji namba moja  alisema maombi ya Askofu yallipokelewa na Mungu  na ndio maana Mungu aliwaongoza wakakataa ahadi vile vile watu mbali mbali walichangia kama alivyoomba na kuongeza kuwa kanisa hilo litakamilika tu kutokana na Padri Manyonyi kuwa na  mahusiano mazuri na watu ,ndio maana wanajitoa pia ni Rafiki  mkubwa wa familia ya Waitara wanaemchukulia kama sehemu ya familia yao.

‎Mama mmoja ambaye hakupenda jina litajwe alisema Padri Manyonyi anashirikina vizuri na watu  hata  wa madhehebu mbali mbali ndio maana walichangia anakubalika na watu wengi ni mpenda amani na haki anayejali watu wote ambaye amejenga urafiki kwenye familia nyingi katika Parokia yake kiasi cha kuwaita hata walio nje ya Tarime kuja kuchangia kanisa na wanaitikia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!