Meneja wa Mradi wa Pamoja wa Vyama vikuu sita vinavyo simamia zao la Korosho (KCJE ) Mohamed Mwinguku amewataka wadau kuwaogopa wale wote wanaobeza shughuli za miradi ya pamoja (joint) kuwaogopa kwasababu ni watu ambao hawapendi kuona wakulima wakipata manufaa ya kilimo chenye tija kwenye mazao yao ambayo wanayasimamia ikiwemo Korosho na pamba.
Ameyaeleza hayo kwenye ziara iliyofanywa na Wanachama wa Mradi wa Pamoja wa Vyama vikuu vya ushirika vinavyolima zao la pamba nchini (TANCCOOP) walipotembelea KCJE kwa lengo la kujifunza kuhusu shughuli ,mifumo na uzoefu katika taasisi hiyo.

Ameongeza kuwa toka kuanzishwa kwa KCJE wamesimamia manunuzi ya pembejeo ya zao la Korosho zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 840 ambazo wamepeleka nchi nzima.
Akieleza mafanikio ya joint hiyo Mwenyekiti wa (KCJE ) Odas Mpunga amesema mafanikio waliyoipata kutokana na umoja huo ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho kutoka tani laki Moja na elfu 40 mwaka 20022 hadi tani laki sita na elfu 18 mwaka 2025,2026.

Mwenyekiti wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vinavyolima zao la Pamba Reonard Lyabalima, amesema eneo ambalo wameona wenzao wamepiga hatua ni uagizaji wa pembejeo kwa pamoja na kuratibu zoezi zima la usambazaji ambapo itawasaidia sana wakulima wao kupata madawa kwa wakati ambapo itasaidia uzalisha kwani kwenye eneo la pamba uzalishaji unapungua.
Ziara hiyo imewakutanisha viongozi na wanachama takribani 21 kutoka TANCCOOPS, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutafuta uzoefu kutoka sekta nyingine za ushirika na kuutumia katika kuboresha huduma kwa wakulima wa pamba.
