Latest Posts

WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA UMEME MANYARA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Manyara, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, limewakamata watu watatu kutoka Kitongoji cha Ndoroboni, Kijiji cha Kiru Six, kwa tuhuma za kuunganisha umeme kinyume cha taratibu na sheria za TANESCO.

Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Samwel Mandar, amesema operesheni hiyo ni sehemu ya msako unaoendelea wa kukagua miundombinu ya shirika, ikiwemo mita za umeme, ili kubaini wananchi wanaotumia umeme kwa njia zisizo halali.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kitengo cha Udhibiti Mapato TANESCO Manyara, Maisha Mchuruza, amesema wananchi wanapaswa kuacha kutumia njia zisizo halali kupata huduma ya umeme na badala yake kufuata taratibu rasmi za kuomba na kuunganishiwa umeme na TANESCO.

Baadhi ya waliokamatwa wamedai kuwa waliunganishiwa umeme na mtu aliyejitambulisha kuwa mfanyakazi wa TANESCO na kuomba fedha kwa ahadi ya kuwaunganishia huduma hiyo. TANESCO imewataka wananchi kuwa makini na watu wanaojifanya wafanyakazi wa shirika na kutoa fedha bila kupata uthibitisho wa taratibu rasmi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!