Latest Posts

OTHMAN- KATIBA YA SASA NDIYO TISHIO KUBWA ZAIDI KWA MUUNGANO

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, ametoa kauli kuhusu mustakabali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitangaza kuwa katiba ya sasa ndiyo tishio kubwa zaidi kwa muungano huo kuliko kitu kingine chochote.

Akizungumza leo Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam chini ya uratibu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Othman amesisitiza kuwa suala la mamlaka huru ni jambo la kukubaliana kwamba mamlaka hayo yanakwenda mpaka wapi, yanaishia wapi, yapi yatasimamiwa na mamlaka ya kati au mamlaka kuu na wanachama wa muungano watakuwa na mamlaka kwa kiasi gani.

Amefafanua kuwa, ingawa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kama mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kiuhalisia TFF haiwakilishi muungano bali inawakilisha ligi ya Tanzania Bara. Wakati huo huo, upande wa Zanzibar umezuiwa kupata uanachama wa FIFA, jambo linalofanya upande mmoja wa muungano kufurahia na kutumia mamlaka ya kimataifa kwa faida yake pekee kinyume na misingi ya usawa wa pande mbili

Mwanasiasa huyo ameonya kuwa kwa sasa muungano unaonekana kuwa shwari kwa sababu tu chama tawala cha CCM kinashika madaraka pande zote mbili, Tanzania Bara na Zanzibar. Hata hivyo, amesisitiza kuwa mfumo wa kikatiba lazima ujengwe kuhimili mabadiliko ya kisiasa pindi chama kingine kitakaposhika madaraka upande wowote.

Ametahadharisha kuwa, kutokana na migongano mikubwa iliyopo kwenye katiba ya sasa, akitokea kiongozi yeyote atakayeamua kusimama kidete na kuifuata katiba hiyo kama ilivyo sasa bila kuifanyia marekebisho, nchi itaingia kwenye vurugu kubwa sana.

Aidha, amefichua siri ya mkwamo wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akieleza jinsi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilivyokiuka makubaliano ya dhati ya mambo matatu yaliyofikiwa kabla ya uchaguzi huo na kusababisha nchi kuingia kwenye uchaguzi bila marekebisho yoyote.

Amebainisha kuwa uzoefu uliopatikana katika chaguzi za miaka ya 2015 na 2020 ulichangia kwa kiasi kikubwa kuunda mchakato wa sasa, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)

Hata hivyo, Othman ameweka wazi kuwa namna uchaguzi wa 2025 ulivyoendeshwa haukuwa tofauti sana na ule wa 2020. Ametaja changamoto zilizoanza tangu hatua ya uandikishaji, makubaliano ya ACT na CCM likiwamo la kuondoa kabisa utaratibu wa kura ya mapema, mpaka kukiukwa kwa baadhi ya makubaliano katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!