Latest Posts

THRDC YATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUHARAKISHWA

Na Jane Turuka, Dar es salaam.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetaka Serikali kuharakisha mchakato wa Katiba mpya, ukisema hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha misingi ya demokrasia, utawala wa sheria na ulinzi wa haki za binadamu nchini.

Wito huo umetolewa leo Septemba 15, 2026, wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Demokrasia. THRDC imesema Katiba mpya inapaswa kutokana na mchakato ulio wazi, jumuishi na shirikishi, unaowapa wananchi nafasi ya kumiliki mchakato huo.

Kwa mujibu wa THRDC, Katiba mpya inapaswa kuimarisha mgawanyo na udhibiti wa madaraka, uhuru wa taasisi, uchaguzi huru na wa haki, haki za binadamu, utawala wa sheria na uwajibikaji wa viongozi na taasisi za umma.

“Baada ya zaidi ya miaka 30 ya udhibiti wa madaraka, uhuru wa taasisi, uchaguzi huru na wa haki, ushindani wa kisiasa wenye mfumo wa vyama vingi, uzoefu wa Tanzania unaonyesha umuhimu wa kufanya mageuzi ya kikatiba, kisheria na kitaasisi yatakayojenga misingi imara ya demokrasia, ikiwemo mgawanyo na usawa, haki za binadamu na uwajibikaji.”, imeeleza taarifa iliyotolewa na mratibu wa kitaifa wa mtandao huo, Wakili Onesmo Olengurumwa.

THRDC pia imetaka Serikali kufanyia kazi mapendekezo ya tume mbalimbali za mageuzi ya kisiasa, kikatiba na uchaguzi, ikiwemo Tume ya Jaji Francis Nyalali, Tume ya Jaji Joseph Warioba na Tume ya Jaji Mohamed Chande Othman, ili mapendekezo hayo yasiendelee kubaki kwenye nyaraka za historia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!