Latest Posts

TAREHE 4 NOVEMBA TWENDE TUKAMTHIBITISHE DKT. NDILITO KUWA MBUNGE WA JIMBO LA CHAMWINO- CHATANDA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 20 Oktoba 2026, amewaomba wananchi wa Kijiji cha Solou, Kata ya Itiso, Jimbo la Chamwino, kujitokeza kwa wingi tarehe 4 Novemba 2026 kumpigia kura Dkt. Nettho Ndijina Ndilito ili kumthibitisha kuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino.

Chatanda ametoa rai hiyo wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika katika Kijiji cha Solou, Kata ya Itiso, akiwahimiza wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na makundi mbalimbali kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kwa kumpigia kura mgombea huyo wa CCM.

Amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa kukipa ushindi wa kishindo, akieleza kuwa umoja, mshikamano na ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuhakikisha chama kinaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Chatanda amewataka wananchi wa Solou kuamka siku ya uchaguzi na kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia kwa kumpigia kura Dkt. Nettho Ndijina Ndilito ili kuhakikisha anapata ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Chamwino.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!