Latest Posts

CBT YARIDHISHWA NA UBORA WA KOROSHO ZINAZOPOKELEWA NA MAMCU

Zaidi ya tani 4,000 za korosho zinatarajiwa kuingia kwenye mnada unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12, 2026, kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU, kinachohudumia wilaya za Nanyumbu, Masasi na Mtwara, mkoani Mtwara.

Akizungumza leo, Oktoba 11, 2026, mara baada ya kukagua maghala mbalimbali yanayopokea korosho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, amesema korosho hizo zina ubora mzuri, huku akikipongeza Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU kwa kusimamia na kuhimiza ubora katika vyama vya msingi.

Aidha, amewasisitiza wakulima kuhakikisha wanapeleka korosho kwenye maghala zikiwa na ubora unaotakiwa ili kupata bei shindani katika minada ya korosho.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!