Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeagiza bendera zake kupepea nusu mlingoti kuanzia tarehe 29 Oktoba 2026 hadi Novemba 4, 2026, ikiwa ni sehemu ya maombolezo na kumbukumbu ya wananchi na wanachama waliopoteza maisha kutokana na matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025.
Agizo hilo limetolewa leo, Oktoba 27, 2026, na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akisoma maazimio maalum yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi leo.
“Bendera za chama zitapepea nusu mlingoti kuanzia Oktoba 29 mpaka Novemba 4,” alieleza Mnyika.
Katika hatua nyingine, Mnyika alibainisha kuwa chama hicho kimeitangaza tarehe 3 Novemba 2026 kuwa siku maalum na rasmi ya kuwakumbuka wote walioteuliwa kufariki dunia kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025, na siku zilizofuata. Katika siku hiyo, CHADEMA kimedhamiria kuwasha mishumaa inayolingana na idadi halisi ya waliopoteza maisha kama ishara ya kuwaenzi na kuwakumbuka wahanga hao.