Latest Posts

NDEJEMBI AAGIZA UCHUNGUZI UFANISI WA VIUATILIFU VYA KOROSHO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameiagiza Wizara ya Kilimo kufanya uchunguzi wa kina kubaini ufanisi wa viuatilifu vya zao la korosho aina ya sulfur vilivyotumika msimu uliopita, ili kubaini iwapo vilikuwa vimechakachuliwa au havikuwa na ubora unaotakiwa.
Akizungumza Leo Novemba 12 na wananchi wa Masasi, Newala na Tandahimba mkoani Mtwara, Ndejembi amesema endapo itabainika kuwa sulfur ya maji haina ufanisi unaohitajika, Wizara iangalie uwezekano wa kurejesha matumizi ya sulfur ya unga ili kuhakikisha wakulima wanadhibiti visumbufu na kuongeza uzalishaji wa korosho.
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amesema tayari timu ya wataalamu imeundwa kufanya tathmini ya kubaini aina ya sulfur inayofaa kwa msimu ujao. Aidha, amewapongeza wakulima wa Tandahimba na Newala kupitia TANECU kwa kuuza zaidi ya tani 70,000 za korosho katika msimu wa minada wa 2026/2027.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!