Latest Posts

MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI YATAKIWA KUTUMIA AKILI UNDE

‎Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, ameitaka Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa, ikiwemo Akili Unde (AI), katika utoaji haki ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia yanayoendelea duniani.
‎
‎Lugangira ametoa wito huo leo Novemba 12,2026 jijini Arusha alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, katika maadhimisho ya miaka 25 ya Mahakama hiyo yenye kaulimbiu isemayo “From Foundation to Future” (Kutoka Msingi Hadi Mustakabali), akisisitiza umuhimu wa mahakama kujiandaa na mahitaji ya miaka 25 ijayo.


‎
‎Amesema ni muhimu kuwekeza katika kuwajengea uwezo watendaji wa mahakama kutumia teknolojia, kuimarisha ushirikiano wa kimahakama kati ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki na kuhakikisha matumizi ya teknolojia yanaongeza upatikanaji wa haki bila kuathiri usawa, uwajibikaji na uhuru wa mahakama.
‎


‎Katika hatua nyingine, Lugangira amesisitiza umuhimu wa mahakama kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazotokana na matumizi ya mitandao ya kijamii na teknolojia za kidijitali, huku akiahidi Mkoa wa Arusha kuendelea kutoa mazingira ya amani na usalama kwa taasisi za kikanda.
‎
‎Pia amewaalika washiriki wa maadhimisho hayo kutembelea vivutio vya utalii vya mkoa huo, ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!