Latest Posts

14 WALIVYONUSURIKA AJALI YA BASI LA KIMOTCO HANANG

Watu 14 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Kimotco iliyotokea eneo la Nangwa, Wilaya ya Hanang’, mkoani Manyara, baada ya basi hilo kupinduka wakati likitokea Arusha kuelekea Singida.

Ajali hiyo imetokea Novemba 19, 2026, majira ya saa 10 jioni katika barabara kuu ya Katesh–Singida, ikihusisha basi lenye namba za usajili T326 DFV aina ya Haighar, lililokuwa likiendeshwa na Shabani Abdallah Nega (60).

Katika ajali hiyo, abiria 14 walipata majeraha na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa za awali za Jeshi la Polisi, ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na uzembe wa uendeshaji.

Akizungumza wakati wa kuwatembelea majeruhi hospitalini, Mkuu wa Wilaya ya Hanang’, Vita Rashid Kawawa, amewapa pole kwa niaba ya Serikali na kuwahakikishia kuwa Serikali ipo pamoja nao, huku akiwatakia uponaji wa haraka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!