Latest Posts

NAIBU WAZIRI REGINA: SERIKALI INAJITAHIDI KUPUNGUZA KERO ZA WATUMISHI

Serikali imesema inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza changamoto zinazowakabili watumishi wa umma nchini, kwa lengo la kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao katika mazingira bora na yenye tija kwa wananchi.

Akizungumza Novemba 18, 2026, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Ndege, amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili watumishi na inaendelea kuzifanyia kazi ili kuboresha ustawi wao na mazingira ya kazi.

Ndege ameyasema hayo wakati akizungumza na walimu wa kike wa shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara, ambapo amesisitiza umuhimu wa kusikiliza changamoto za watumishi na kuzitafutia ufumbuzi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Aidha, amewahimiza walimu kuendelea kuwa na moyo wa kujituma, kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kutekeleza majukumu yao kwa weledi, akieleza kuwa serikali inaendelea kujenga mazingira yatakayowawezesha watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!