Latest Posts

BENKI YA DUNIA YAIKUBALI MIRADI YA MAJI, PANGANI YAUPIGA MWINGI

 

 

PANGANI YAUPIGA MWINGI

Wataalamu wa Wizara ya Maji na wawakilishi wa Benki ya Dunia wamekagua mradi wa maji wa Sange na Zahanati ya Masaika wilayani Pangani na kuridhishwa na utekelezaji wake.

Kazi hiyo inafanyika mkoani Tanga ikiwa ni ufuatiliaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira iliyotekelezwa kupitia fedha za programu ya lipa kwa matokeo (PforR) katika Sekta ya Maji.

Mradi wa maji Sange una thamani ya shilingi milioni 540 na umeanza kuhudumia wananchi, ambapo utekelezaji wake ni asilimia 90.

Ujenzi wa mradi huo umehusisha tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 5000, ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukuma maji, ujenzi wa vituo vya umma vya kuchotea maji 13, na ulazaji wa mabomba zaidi ya mita 9,900.

Kwa upande wa usafi wa mazingira katika Zahanati ya Masaika, kazi imehusisha ujenzi wa kichomea taka, eneo la kitakasa mikono, ujenzi wa vyoo vya watumishi, matundu ya vyoo kwa huduma ya wagonjwa, ujenzi wa mnara, na ununuzi wa tanki la kuhifadhia maji.

Wilaya ya Pangani kwa sasa imefikia asilimia 92 ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama. Wananchi wametoa shukrani kwa serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kufanikisha huduma ya maji kwa watu wote.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!