Latest Posts

CITIBANK YAAHIDI KUENDELEZA UFADHILI NA USHAURI WA KIFEDHA KWA TANZANIA

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikishirikiana na Benki ya Citibank ya Marekani kwa zaidi ya miaka 35, ikipokea ushauri wa kifedha kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Waziri Mkuu aliyasema hayo siku ya Jumanne, Septemba 24, 2024, alipokutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Citibank, Bw. John Dugan, katika makao makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani.

“Serikali ya Tanzania inatoa shukrani za dhati kwa Citibank kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa nchi yetu, ikiwemo upatikanaji wa mikopo na ushauri wa kifedha. Citibank imekuwa ikifadhili miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kujengwa nchini,” alisema Waziri Mkuu.

Aliongeza kuwa benki hiyo imekuwa ikikopesha kampuni zinazojenga Reli ya Kisasa (SGR) na pia kufadhili moja ya loti za ujenzi wa reli hiyo. Vilevile, Citibank imechangia katika uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Pemba.

Waziri Mkuu Majaliwa pia alitaja jinsi Citibank ilivyoisaidia Tanzania wakati wa changamoto ya uhaba wa mafuta, kwa kuwasaidia wafanyabiashara kupata mafuta kwa bei nafuu, jambo lililosaidia kuimarisha sekta ya uchumi wa nishati.

Zaidi ya hayo, benki hiyo, kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Marekani (U.S. International Development Finance Corporation), imekuwa ikitoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo, hasa wanawake, kuwapa fursa za kujiendeleza kiuchumi na kumiliki biashara zao binafsi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Citibank, Bw. John Dugan, aliahidi kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo, kama ambavyo imefanya kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!