Latest Posts

DC ANGELINA APOKELEWA RASMI SERENGETI, AAHIDI KUFANIKISHA DIRA YA RAIS SAMIA

Mkuu mpya wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Bi. Angelina Marko, ameahidi kushirikiana kikamilifu na viongozi pamoja na watendaji wa wilaya hiyo katika kuhakikisha utekelezaji wa maagizo na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu Evans Mtambi, Bi. Angelina atoa shukrani kwa Rais Samia kwa kumuamini na kumpa jukumu hilo la uongozi.

“Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa heshima hii kubwa ya kuniteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti. Ninaahidi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na viongozi wote kuhakikisha tunaleta maendeleo Serengeti,” alisema Angelina.

Bi. Angelina ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti, pia alimpongeza mtangulizi wake, Kemirembe Lwota, kwa kumwongoza vyema katika misingi ya utendaji bora, akisema atajenga juu ya msingi aliouacha.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mara, Mkuu wa Mkoa Kanali Mtambi aliwataka wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi, ikiwemo migogoro ya ardhi na huduma za kijamii, badala ya kuzisababisha au kuzidumaza.

“Tunataka viongozi mkawe suluhisho, sio sehemu ya tatizo. Nendeni mkawahudumie wananchi kwa haki, weledi na kwa moyo wa kizalendo,” alisema Mtambi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!