Latest Posts

DC BABATI AKEMEA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO NA VIJANA

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mheshimiwa Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amekemea vikali vitendo vya kikatili kwa makundi ya watoto na vijana yanapelekea kukatishwa kwa ndoto zao za msingi.

Mheshimiwa Kaganda ametoa nasaha hizi katika uzinduzi wa kampeni ya “Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa” iliyofanyika katika Kata ya Bagara, uwanja wa Shule ya Sekondari Babati Day, ambapo kampeni hiyo iliwakutanisha wanafunzi mbalimbali kutoka shule za sekondari na baadhi ya wanachuo.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Kaganda amewataka wanafunzi hao kujiepusha na starehe zinazowapelekea kuingia katika mitego ya kuharibiwa pamoja na tamaa ya vitu mbalimbali, kwa pande zote mbili: wanafunzi wa kike na wa kiume, kwani makundi yote yapo hatarini kuharibiwa.

Aidha, Mheshimiwa Kaganda amewataka jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wazazi wa wanafunzi, ili elimu hizo ziwasaidie kuwakomboa wanafunzi hao na makundi ya vijana yanayokaribia kuharibiwa ili kuwa na kizazi endelevu katika uchumi.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara SACP Ahmed Makarani ameeleza kuwa kampeni hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha miezi sita mfululizo, wakiwalenga wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, shule za msingi, vyuo vikuu pamoja na vyuo vya kati. “Ni jukumu letu sisi, wananchi, viongozi wa dini, na wadau mbalimbali, tuwaambie wasije wakajiingiza katika makundi hatarishi baadae wakahatarisha maisha yao,” amesema Kamanda Makarani.

Halikadhalika, Afisa Maendeleo Mkoa wa Manyara ameyagusia pia makundi ya wanaume wadogo kulindwa, kwani bado ni miongoni mwa makundi yanayopata changamoto ya kulawitiwa, na kuwataka watoto pamoja na wazazi na viongozi wa dini kushirikiana kukomboa kundi hili katika makuzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!