Na Stephano Mango, Tunduru
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Simoni Chacha amewataka watendaji wa kata na vijiji wasiwe na tamaa ya kuingiza maslahi binafsi katika kupata watu wanaohitaji Mikopo, hivyo kila mmoja afanye kazi kwa kufuata kanuni na taratibu zilizopo.
Chacha ametoa wito huo wakati anafungua mafunzo yanayohusu Sheria na Kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo ya Asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu katika ukumbi wa Skyway Mjini Tunduru.
Mafunzo haya yamelenga kuimarisha uelewa wa sheria zinazosimamia utoaji wa mikopo. Mkuu wa Wilaya amesisitiza umuhimu wa mikopo katika kuendeleza uchumi wa jamii na kuwapa nguvu wajasiriamali.
Pia amesisitiza kwa Wajumbe wote kuhusu maadili na uadilifu akisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ana lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji na siyo kuwapa watu wasio stahili.
Katika mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Tunduru Bi. Jecelyne Mganga Amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inatarajia kutoa Mikopo ya Asilimia 10 kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu katika maeneo yote ndani ya Wilaya ya Tunduru kiasi cha Tsh 726,119,965.3.
Afisa Maendeleo ametambulisha Kamati za huduma ya mikopo ya Kata pamoja na Kamati ya ya Uhakiki ngazi ya Wilaya sambamba na Kamati ya huduma za Mikopo ya Wilaya.
Bi. Mganga alieleza kuwa Kamati ya Uhakiki ina wajumbe 6 ambao wanaongozwa na Katibu Tawala Wilaya pamoja na wajumbe watatu kutoka kwenye vyombo vya Usalama ambao ni Polisi, PCCB na Usalama wa Taifa na katibu wake ni Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii na Mjumbe mmoja kutoka mkoani