Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Kaspar Kaspar Mmuya amewataka Watendaji wa Serikali za Mitaa/Vijiji kuhakikisha taarifa za Anwani za Makazi zinahakikiwa kikamilifu kwa kuwa ni muhimu kwa Ustashi wa jamii zetu na serikali kwa ujumla katika kupanga mipango mbalimbali.
Msuya ameyabainisha hayo leo Jumatatu Mei 26,2025 Jijini Dodoma wakati wa Halfa ya uzinduzi wa zoezi la uhakiki wa taarifa za Anwani za makazi halmashauri ya Jiji hilo pamoja na utoaji wa Mafunzo kwa Watendaji wa Serikali za Mitaa/ Vijiji na Wenyeviti wa Mitaa/Vijiji kupitia usimaminzi wa Wizara ya Mawasiliano na teknolojia ya habari.
RAS Mmuya amesema hawategemi kuona Mtendaji yeyote ana taarifa zenye mapungufu katika mtaa/Kijiji chake nackuongeza kuwa kila mtendaji ana wajibu wa kuhakikisha kila mkazi katika eneo lake amesajiliwa kwa kuwa jukumu la Kutunza daftari la wakazi ni la kila Mtendaji wa Mtaa/Kijij.

Hata hivyo amesema miongoni mwa masuala yanayoisukuma nchi kuwa na mfumo imara wa Anwani za Makazi ni pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025/2050 inayoandaliwa na Agenda 2030 na Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo endelevu.
“Masuala hayo yanasisitiza matumizi ya teknolojia sahihi katika kuchochea ukuaji wa Uchumi hususan Uchumi wa kidijitali, ili kujenga jamii zenye Maisha bora na maendeleo endelevu ili kufikia Uchumi kamili wa kidijitali ni lazima kama nchi tuwe na mfumo imara wa Anwani za Makazi utakaowezesha wananchi kutambuana na kuweka mazingira rafiki na salama ya kufanya biashara mtandao,” ameeleza RAS Mmuya
Kwa upande wake Mwakakilishi Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye yeye ni Mkurugenzi Msaidizi Rasilimaliwatu Mawasiliano Josephine Mwaijande amesema nchi imeanza kunufaika na uwepo wa Mfumo wa Anwani za Makazi ikiwa ni pamoja “Disemba 2023 tulishuhudia namna taarifa za Anwani za Makazi zilivyosaidia kubainisha makazi yaliyoathirika na Maporomoko ya tope kule Hanang,”
“ Vilevile, Aprili, 2024 taarifa hizi zilitumika kubainisha waathirika wa Mafuriko katika Wilaya za Rufiji na Kibiti na hivyo kurahisisha shughuli za uokozi na kurejesha hali, zipo taasisi ambazo zinatumia taarifa hizi kufikisha huduma majumbani ikiwemo Shirika la Posta na Kampuni ya simu ya TTCL ambayo inatoa huduma za internet majumbani,”
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amewahimiza Wananchi wa Jiji hilo na Mkoa mzima kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kuhakiki taarifa za Anwani zao.
“Ni matarajio yangu kuwa baada ya zoezi hili, kila mmoja ataweza kufahamu Anwani yake ya Makazi na kujenga utamaduni wa kujitambulisha kwa kutumia Anwani hiyo,”